Tanzania kasi ya uvunaji misitu kubwa kuliko upandaji


Usivune mti kama hujapanda miti
WASTANI wa hekta 25,000 hupandwa kila mwaka ikilinganishwa na kiwango cha hekta 91,276 za misitu zinazotoweka kila mwaka.Hayo yemeelezwa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, wakati akijibu swali bungeni, ambapo alisema serikali itahakikisha kuna kuwepo na uwiano kati yauvunaji utakaoendana na utunzaji wa mazingira kwenye maliasili ya misitu.Alisema utaratibu huo utakapoanza kutumika, hakutafanyika uvunaji wowote katika wilaya yoyote ile, hadi wilaya husikaitakapokuwa imetayarisha mpango wa usimamizi wa misitu ili mazingira ya kila wilaya yazidi kuboreshwa.

”Mazingira ya kila wilaya yaendelee kuboreshwa na kila mvunaji wa mazao ya misitu katika misitu ya asili anatakiwa kulipia asilimia tano ya ushuru wa mazao husika kwenye mfuko maalum ambao fedha zake zinatumika kwa shughuli za kupandamiti mingine ili kuendeleza misitu,” alisema Maige.Alieleza kuwa serikali kupitia miradi ya usimamizi shirikishi wa misitu, imesaidia kuweka rasilimali hiyo katika usimamizi madhubuti chini ya serikali za vijiji na kwamba jumla ya hekta 2,060,000 zinasimamiwa na vijiji 1,102.Alisema kuwa mwaka 2006, serikali ilitoa kitabu cha mwongozo wa uvunaji endelevu na biashara ya mazao ya misitu, ambao unaweka utaratibu madhubuti utakaofuatwa katika Uvunaji.

Awali, Mbunge wa Liwale Chande Hassani Kigwalilo, katika swali lake alitaka kujua utata unaosababishwa na biashara ya magogo na njia ambazo seerikali itazitumia kukabiliana na hali hiyo.

Advertisements

About sharuvembo

Compaign again poverty
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s